• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatekeleza majukumu ya nchi kubwa katika mchakato wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-10-01 19:14:53

    Mkutano wa kilele wa baraza la usalama kati ya China na Afrika ulifanyika mwanzoni mwa mwezi wa Septemba, ambapo rais Xi Jinping wa China alisema, amani na maendeleo ni mada kuu ya zama ya leo, na pia ni suala kuu la zama hiyo linalohitaji jumuiya ya kimataifa kubeba majukumu ya kihistoria, kujibu suala hilo na kuonesha uwajibikaji kupitia mshikamano, busara na ujasiri.

    Dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ambayo haikuwepo zamani. Jamhuri ya watu wa China iliyopita miaka 69 ikiwa mlinzi wa utaratibu wa kimataifa na mtekelezaji wa mfumo wa pande nyingi, jinsi inavyokabiliana na sauala kuu la amani na maendeleo itafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa.

    Ili kulinda amani, wakati China inapohimiza maendeleo imara ya uchumi na jamii ya ndani, imekuwa nguvu muhimu ya operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. Katika miaka 28 iliyopita, China imetuma polisi na askari elfu 37 kushiriki kwenye operesheni za kulinada amani za umoja huo, 21 kati yao walifariki wakati wa operesheni hizo. China imekuwa nchi ya pili kwa kutoa fedha nyingi zaidi katika operesheni hizo, na pia imekuwa nchi inayowapeleka walinzi wengi zaidi wa amani kati ya nchi tano wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Msemaji wa idara ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Bw. Nick Birnback amesema, China, ikiwa mjumbe wa kudumu wa baraza hilo, imekuwa ni mfano mzuri kwa nchi nyingine kwa sababu baadhi ya nchi wanachama hawataki kutoa nguvu kwa shughuli ya ulinzi wa amani za umoja huo. Ushiriki wa upigaji kura na kulipa gharama za operesheni hizo ni muhimu, lakini China kutuma walinzi wa amani katika sehemu hizo zenye hali ngumu ni muhimu zaidi.

    China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, inafahamu umaskini una maana gani kwa nchi moja, ukanda mmoja na familia moja. Takwimu mpya zinaonesha kuwa, tangu China itoe pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" mwaka 2013, nchi na mashiriki zaid ya 100 ya kimataifa yamesaini makubaliano na China, na thamani ya biashara kati ya China na nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo hilo imezidi dola trilioni 5 za kimarekani, huku uwekezaji wa jumla katika maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwenye nchi hizo ukizidi dola bilioni 28.9 za kimarekani na kutoa nafasi laki 2.44 za ajira na mapato ya kodi za dola zaidi ya bilioni 2 za kimarekani kwa huko.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameipongeza China kwa ushirikiano wa kunufaishana na Afrika kupitia pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema, pendekezo hilo lina uwezo mkubwa wa ushirikiano ambao utanufaisha nchi zinazoshiriki, na hii pia ni sababu ambayo Kenya na nchi za Afrika kwa ujumla zinapenda kuimarisha ushirikiano na China.

    Katika wimbi la maendeleo ya historia na zama za sasa, hakuna nchi inayoweza kujitenga na nchi nyingine. China ikiwa nchi inayofungua mlango wazi kwa kasi ya juu zaidi na kiasi kikubwa zaidi, watu wataona kuwa nchi hiyo itaendelea kutia nguvu mpya na kutoa mchango mpya katika shughuli ya amani na maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako