• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yalaani Marekani kwa kuendeleza vikwazo dhidi yake

    (GMT+08:00) 2018-10-01 19:24:54

    Korea Kaskazini imeilaani Marekani kuendeleza na vikwazo dhidi yake wakati wajumbe wa pande hizo mbili walipofanya mazungumzo.

    Hayo yamo kwenye makala iliyotolewa jana kwenye gazeti la Rodong Simun la Korea Kaskazini. Makala hiyo imesema, tarehe 14 mwezi uliopita waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo alisema nchi yake imeweka vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kwa ajili ya kutimiza peninsula ya Korea isiyokuwa na silaha za nyuklia, na kusisitiza kuwa Marekani itaendelea kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa. Katika taarifa ya pamoja ya Korea Kaskazini na Marekani iliyosainiwa nchini Singapore, pande hizo mbili ziliahidi kujenga uhusiano mpya unaolingana na matarajio ya amani na ustawi ya watu wa nchi hizo mbili. Habari nyingine zinasema, Korea Kusini na Korea Kaskazini leo zimeanza kuondoa mabomu ya ardhini kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kufanya juhudi kutekeleza makubaliano ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako