• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Bei ya maziwa iko imara licha ya mabadiliko ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-10-01 19:26:39

    Kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi, bei ya maziwa imebakia imara licha ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Wakulima wa maziwa na wasindikaji wa maziwa wanasema lita moja ya maziwa ghafi, tangu mwanzo wa mwaka hawajapata chini ya Shs800, mbali na kawaida.

    Uganda ndio muuzaji mkubwa wa nje wa maziwa na bidhaa za maziwa, na thamani ya mauzo ya nje ya sasa iko karibu dola milioni 80 sawa n ash bilioni 284.8 ya Uganda.

    Kwa mujibu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Maziwa, matumizi ya maziwa ya kila mwaka nchini Uganda yameongezeka kutoka lita 25 mwaka 1986 hadi lita 62 mwaka 2017.

    Ni asilimia 33 tu ya maziwa inayonunuliwa inasindikwa na asilimia 67 kuuzwa ghafi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako