• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu zaidi ya laki 1.9 wanahitaji msaada baada ya tetemeko na tsunami Indonesia

    (GMT+08:00) 2018-10-02 08:55:31

    Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema watu zaidi ya laki 1.9 wanahitaji msaada wa kibinadamu, baada ya tetemeko na tsunami kuleta madhara kwenye jimbo la Central Sulawesi nchini Indonesia.

    Zaidi ya nusu ya watu hao wametajwa kuwa ni watu wa vijijini na wengine ni wa mijini, na msaada unaotakiwa zaidi ni chakula, maji safi na malazi.

    Tetemeko lenye nguvu lililotokea kwenye kina kifupi kwa mfululizo likiwa na nguvu ya 6.0, 7.4 na 6.1 mtawalia lilitokea katika jimbo hilo na kusababisha tsunami iliyoleta madhara.

    Idara ya kukabiliana na maafa ya Indonesia imesema, mpaka sasa watu 1,203 wamefariki, 540 wamejeruhiwa na wengine zaidi ya elfu 16 wamekimbia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako