• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa makubaliano ya biashara huria na utambulisho wa kidigitali barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-02 08:55:54

    Katibu mkuu wa kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa Bibi Vera Songwe, amehimiza kuwepo kwa eneo la biashara huria la Afrika (AfCFTA), utambulisho wa kidigitali na fursa za uwekezaji, kama sekta zinazohitaji kipaumbele barani Afrika.

    Akiongea kwenye vikao vilivyofanyika sambamba na mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Bibi Songwe ametaja maeneo hayo ambayo yanaweza kuchochea maendeleo ya bara la Afrika.

    Akifafanua maana ya utambulisho wa kidigitali, Bibi Songwe amesema utambulisho huo utawasaidia watu kuwa na utambulisho wa kidigitali, ili waweze kupata huduma kwa urahisi kupitia mtandao wa internet, kama vile huduma za fedha, fursa za uchumi, simu za mkononi na internet, huduma za serikali na hata mchakato wa kidemokrasia.

    Pia amezipiongeza Kenya, Mauritania na Senegal kuwa mfano wa kuigwa kwenye kuweka mazingira mazuri ya kuunga mkono uwekezaji kwenye sekta ya nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako