• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano unahitajika kukabiliana na tatizo kubwa la watu kupoteza makazi.

    (GMT+08:00) 2018-10-02 08:56:21

    Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNCHR Bw. Filipo Grandi, amezitaka nchi mbalimbali kufanya kazi kwa karibu zaidi kutafuta njia za kutatua tatizo la watu wanaomba hifadhi, ili kuwe na utatuzi halisi wa tatizo la watu wanaomba hifadhi.

    Akihutubia mkutano wa kamati kuu ya UNHCR mjini Geneva, wakati idadi ya watu waliokimbia makazi yao duniani imeongezeka na kufikia milioni 68.5. ikiwa ni pamoja na wakimbizi milioni 25.4 na watu milioni 40 waliokimbia makazi yao ndani ya nchi.

    Amesema tangu aingie madarakani mwaka 2016, migogoro ya ndani na misukosuko imeongezeka, ikichochewa na uhasama wa kikanda na kimataifa, na kuchangiwa na umaskini, watu kutengwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati huo huo kauli za kisiasa zimekuwa za kikatili, na kuhimiza ubaguzi, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni.

    Pia ametoa mwito wa makubaliano kuhusu wakimbizi kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni njia nzuri ya kukabiliana na suala la wakimbizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako