• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AMISOM yatoa mafunzo kwa polisi kuhusu kudhibiti matishio ya ugaidi katika vituo vya ukaguzi nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-10-02 09:13:51

    Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema imewafunza polisi 100 kwa ajili ya kupunguza matishio ya ugaidi yanayoweza kutokea kwenye vituo vya ukaguzi wa magari nchini Somalia.

    Tume hiyo imetoa taarifa mjini Mogadishu ikisema mafunzo hayo yamelenga kuongeza njia za kusimamia vituo vya ukaguzi kwa kupitia mfumo wa kujibu haraka vitendo vya kigaidi.

    Kaimu kamishna wa polisi wa AMISOM Bi. Christine Alalo amesema mafunzo hayo yanalenga kuwafanya polisi wa AMISOM na wa Somalia wafanye maandalizi kwa ajili ya muda wa mpito. Amewataka polisi hao watumie vizuri ujuzi walioupata kwenye mafunzo, ili kuboresha usalama wa Mogadishu na miji ya maeneo mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako