• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jose Mourinho: Asema hahofii kufukuzwa kazi Manchester United

    (GMT+08:00) 2018-10-02 10:13:30

    Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema hana wasi wasi kufuatia tetesi zilizozagaa kuwa huenda akafukuzwa kazi, na kwamba hata hivyo haogopi kutimuliwa kutokana na kipigo cha magoli 3-1 kutoka kwa West Ham United.

    Mourinho pia amekana kuthibitisha kuwa alikutana na uongozi wa klabu baada ya kufungwa na West Ham, na kwamba hivi sasa anaiandaa timu kwa ajili ya mechi ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Valencia usiku wa leo.

    Katika hatua nyingine kuna habari zimeenea kuwa Zinedine Zidane huenda akachukua wadhifa wa kuifundisha United endapo Mourinho ataondoka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako