• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la China lapinga vikali uchochezi wa Marekani katika Bahari ya Kusini ya China

    (GMT+08:00) 2018-10-02 18:14:44

    Jeshi la China limeeleza kupinga vikali kuingia kwa manowari ya kivita ya Marekani kwenye bahari inayozunguka visiwa na miamba katika Bahari ya Kusini ya China.

    Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Wu Qian amesema, manowari hiyo iliingia kwenye Bahari ya Kusini ya China jumapili iliyopita, na kwamba meli ya jeshi ya China ilifuata utaratibu wa utambulisho na uhakiki kama sheria inavyoelekeza. Amesisitiza kuwa China ina mamlaka isiyopingika juu ya visiwa vilivyoko kwenye Bahari ya Kusini ya China.

    Amesema hivi sasa, kutokana na juhudi za pamoja za China na nchi za ASEAN, hali katika Bahari ya Kusini ya China inaendelea kuwa ya utulivu na kufuata mwelekeo mzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako