• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wengi watalii katika siku za mapumziko za sikukuu ya taifa

    (GMT+08:00) 2018-10-02 18:21:36

    Kila ifikapo sikukuu ya taifa, wachina wengi wanakwenda kutalii katika sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi, kwani wana siku 7 za mapumziko. Taasisi ya utafiti wa utalii ya China inakadiria kuwa, katika siku moja tu ya jana, idadi ya watalii nchini China ilifikia milioni 122, ambalo ni ongezeko la asilimia 7.54 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

    Jana tarehe mosi Oktoba ni siku ya 69 ya kuzalishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Siku hiyo hafla ya kupandisha bendera ya taifa katika Uwanja wa Tian'anmen iliwavutia watalii laki 1,45.

    Ili kuwavutia watalii, mji mbalimbali nchini China imeandaa shughuli mbalimbali. Mjini Beijing sikukuu ya 20 ya kimataifa ya utaili ilifunguliwa jana asubuhi, na vikundi 30 vya waigizaji kutoka nchi mbalimbali duniani vifanya maonesho mazuri kwa ajili ya watalii. Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya utalii ya Beijing Bibi Wang Yue anasema,

    "Tumeanzisha sikukuu hiyo ya mwaka huu ambayo pia ni sikukuu ya taifa, ili kuonesha nia na imani yetu kuhusu maendeleo ya utalii mjini Beijing. Aidha, tumejitahidi kuboresha mazingira ya utalii, ili kuwawezesha watalii kutoka sehemu mbalimbali wajionee uzuri wa mji wetu."

    Wakati huo huo, Shirika la Utalii la Xiecheng linakadiria kuwa, wachina zaidi ya milioni 7 watatalii nchi za nje katika siku saba za mapumziko za sikukuu ya taifa. Mfanyakazi wa shirika hilo Bibi Zhai Mengna amesema, licha ya Marekani, Japan, nchi za Ulaya na Asia ya kusini mashariki ambazo ni nchi watalii wa China wanazopendelea zaidi, mwaka huu watalii wa China pia wamechagua kutalii katika nchi mpya kadhaa. Anasema,

    "Mwaka huu nchi nane mpya zimetangaza kusamehe visa kwa watalii wa China. Nchi hizo zikiwemo Qatar, Bosnia, na Belarus zinapendwa sana na wachina. Aidha, kutokana na mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, wachina wengi wameenda kutalii katika nchi za Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako