• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushindani wa wachina ni uchapa kazi

    (GMT+08:00) 2018-10-02 18:22:00

    China imepata maendeleo na mafanikio makubwa sana katika miaka 40 iliyopita ambayo yanategemea sera na mikakati ya ufunguaji mlango wazi na mageuzi pamoja na uchapa kazi wa wananchi. Uchapa kazi wa Wachina umebadilisha familia, jamii na taifa. Uchapa kazi, ufanisi na uvumilivu umekuwa kiini cha ushindani wa wafanyakazi wa China.

    Mwanzilishi mwenzi wa kampuni ya mitaji ya Sequoia Bw. Michael Moritz ametoa makala kwenye gazeti la Financial Times akitoa wito kwa wafanyabiashara wa Silicon Valley kuiga mfano wa wenzao wa China. Amesema, viongozi wa kampuni nchini China wanaanza kazi saa mbili asubuhi na wanaedelea na kazi hadi saa nne usiku. Wengi wao wanafanya kazi siku sita kwa wiki, na baadhi yao wanafanya kazi hata siku saba. Wahandisi huanza kazi saa nne asubuhi na kumaliza kazi usiku wa manane. Mbali na siku za mapumziko ya mwaka wa jadi wa kichina na siku ya taifa, wengi wao wanapumzika siku chache tu kwa mwaka.

    Mbali na wafanyakazi na wafanyabiashara, watumishi wa serikali ya China pia ni wachapa kazi. Ripoti ya uchunguzi wa uaminifu iliyotolewa na Edelman mwaka 2018 imeonesha kuwa, kiwango cha uaminifu kwa serikali cha wananchi wa China kimefikia asilimia 84 huku kiwango hicho cha kundi la wananchi wenye elimu ya juu na mapatato ya juu kikifikia asilimia 89, ambacho ni cha juu zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako