• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 9 wa Al Shabaab wauawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Marekani nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-10-02 18:45:56

    Wapiganaji tisa wa kundi la Al Shabaab wameuawa na mwingine kujeruhiwa katika shambulizi la anga lililofanywa na kikosi maalum cha Marekani kusini mwa Somalia.

    Shambulizi hilo limefanyika jana kaskazini mashariki mwa mji wa Kismayo, na kwamba hakuna raia waliouawa au kujeruhiwa.

    Marekani imeongeza operesheni zake nchini Somalia katika mwaka mmoja uliopita na kusababisha vifo vya wapiganaji kadhaa wa kundi la Al Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako