• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Serikali kuongeza uwekezaji sekta ya mifugo

    (GMT+08:00) 2018-10-02 19:14:48

    Serikali ya Rwanda imeanzisha mpango wa miaka mitano wa kuendeleza sekta ya mifugo nchini humo na kuongeza mapato ya wakulima.

    Maafisa wanasema mpango huo utapunguza gharama za bidhaa za mifugo.

    Ili kufanikisha mpango huo serikali itahitaji dola milioni 310 na kiwango kikubwa cha fedha hizo kinatarajiwa kutoka kwa sekta ya kibinafsi.

    Uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza tani 663,000 za uzalishaji wa nyama kila mwaka, lita bilioni 2.2 za maziwa na mayai bilioni 1.9.

    Mkurungezi mkuu wa sekta ya mifuzo kwenye wizara ya kilimo Theogene Rutagwenda,amesema pia sekta ya ufugaji nguruwe itaimarisha lengo la baadaye likiwa ni kuhakikisha chakula cha kutosha nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako