• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Choppies yafungua tawi Ongata Rongai

    (GMT+08:00) 2018-10-02 19:07:51

    Kampuni ya Maduka ya Choppies kutoka Botswana itafungua tawi jipya katika mtaa wa Ongata Rongai nchini Kenya, katika jumba ambalo awali lilikuwa na duka la Uchumi.

    Choppies inaingia kwenye ushindani na maduka ya Tuskys, Tumaini na Cleanshelf kwenye mtaa huo wenye watu wengi.

    Katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka 2017 Choppies ilitangaza kuwa itawekeza dola milioni 2.27 kufungua maduka mapya nchini Kenya.

    Maduka ya Uchumi na Nakumatt ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto za kifedha yamefunga matawi yake mengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako