• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bomba la gesi kati ya Tanzania na Uganda kuanza 2021

    (GMT+08:00) 2018-10-02 19:10:14

    Shirika la maendeleo ya gesi nchini Tanzania limesema lina imani kuwa mradi wa bomba la gesi kati yake na Uganda utaanza mwaka 2021.

    Meneja Mkurungezi wa shirika hilo Kapuulya Musomba amesema makampuni 29 yametuma maombi ya kufanya utafiti na kujenga bomba hilo.

    Utakapokamilika mradi huo utawezesha gesi kusafirishwa kutoka Tanzania hadi magharibi mwa Uganda ili kutumika kwenye viwanda vya chuma.

    Alisema wanatarajia utafiti kukamilika mwezi Juni mwaka ujao huku shughuli za kutafuta ufadhili zikiendelea hadi mwaka 2020.

    Tanzania na Uganda tayari zimesaini makubaliano ya ujenzi wa bomba hilo kuanzia mjini Dar es Salaam tkupitia bandari yaTanga hadi Mwanza na baadaye kuingia nchini Uganda.

    Tanzania inajiandaa kuwa mchangiaji mkuu wa kawi kwenye kanda ya Afrika Mashariki huku gesi yake ikiwa ni futi trilioni 57 za ujazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako