• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa barabara inayounganisha Msumbiji na Tanzania wazinduliwa

    (GMT+08:00) 2018-10-03 09:17:58

    Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji jana aliweka jiwe la msingi mkoani Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, linaloashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara itakayounganisha Msumbiji na Tanzania.

    Akihutubia uzinduzi wa mradi huo rais Nyusi amesema ujenzi huo unamaanisha kuwa ndoto ya viongozi wa zamani na wananchi wa nchi mbili imetimia. Ameongeza kuwa barabara hiyo itahimiza shughuli za biashara kati ya Msumbiji na Tanzania, na kusaidia kuondoa umaskini.

    Mradi huo ukiwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja matatu umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika na kujengwa na kampuni ya China, na utahimiza usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kuchangia utalii wa kimazingira, unaotarajiwa kukuza uchumi wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako