• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM yatoa wito kwa Afrika kuiwekea tena mikakati mipango ya ukataji miti

    (GMT+08:00) 2018-10-03 09:36:58

    Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa serikali za nchi za Afrika kuiwekea tena mikakati mipango yao ya ukataji miti na uharibifu wa mazingira.

    Wito huo ulitolewa jana na Mshauri wa Kiufundi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNDP Kanda ya Afrika, Elsie Attafuah, na kuzitaka serikali kuunganisha pamoja mbinu zao kwa lengo la kunufaisha jamii. Akiongea kwenye mkutano wa kubadilishana maarifa juu ya kukabiliana na ukataji wa miti mjini Nairobi, Attafuah amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kutumia mbinu zitakazoleta manufaa kwa jamii kutokana na maliasili kupitia matumizi mazuri ya ardhi na kupunguza ukataji miti.

    Amesema mbinu zinapaswa kuleta mabadiliko, mshikamano na kufungamanisha na Mchango wa Maamuzi ya Kitaifa NDC na kupunguza hewa chafu kutokana na mpango wa ukataji miti na uharibifu wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako