• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watoa msaada wa dharura wa fedha kwa Indonesia kutokana na tetemeko kubwa la ardhi

    (GMT+08:00) 2018-10-03 09:56:23
    Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa utatenga dola milioni 15 za kimarekani kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.4 katika kipimo cha Richter lililotokea huko Sulawesi, Indonesia.
    Mratibu wa Utoaji wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Bw. Mark Lowcock amesema, fedha hizo zinazokusanywa kutoka Mfuko wa msaada wa dharura zitasaidia mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo tayari yamefika eneo la maafa kutoa msaada kwa kufuata vipaumbele vinavyowekwa na Serikali ya Indonesia, pamoja na maelfu kadhaa ya wahanga.
    Bw. Lowcock amesema fedha hizo zitatumiwa kwa kufuata maagizo ya serikali ya Indonesia yanayohusisha usambazaji wa vitu, makazi, maji safi ya kunywa, huduma za afya, uratibu na usimamizi wa kambi pamoja na mambo ya ulinzi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako