• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Jumapili

    (GMT+08:00) 2018-10-03 09:57:18

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo atasafiri kwenda Korea Kaskazini kwa mazungumzo zaidi kuhusu kuondoa silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea.

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bi. Heather Nauert amesema Bw. Pompeo atakuwa na mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un Jumapili, na kuongeza kuwa Bw. Pompeo pia atakwenda nchini Japan, Korea Kusini na China kuanzia tarehe 6 hadi 8 Oktoba ili kuelezea matokeo ya ziara yake hiyo nchini Korea Kaskazini. Amesema hii ni mara ya nne kwa Bw. Pompeo kwenda nchini Korea Kaskazini ndani ya mwaka mmoja, na kwamba bado kuna safari ndefu, lakini wote wana matarajio makubwa juu ya hatua zitakazochukuliwa katika mazungumzo haya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako