• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hoteli za kimataifa zaangazia sekta ya huduma ya Afrika kutokana na ukuaji wake endelevu

    (GMT+08:00) 2018-10-03 10:30:44

    Sekta ya huduma ya Afrika ambayo ilikumbwa na hali mbaya kutokana na wasiwasi wa kisiasa, mashambulizi ya kigaidi na mlipuko wa magonjwa na kushindwa kuwa na ukuaji mzuri, sasa inavutia ufuatiliaji wa hoteli za kimataifa.

    Wakiongea kwenye mkutano wa pembezoni mwa Kongamano la Uwekezaji wa Hoteli la Afrika kwa mwaka 2018 mjini Nairobi, watendaji kutoka hoteli mbalimbali za kimataifa wamesema sekta za huduma na usafiri za Afrika zinazobadilika kwa kasi zina matarajio makubwa ya kurejesha uwekezaji. Mkurugenzi wa Hoteli za Acco za Mashariki ya kati na Afrika Olivier Granet amesema bara la Afrika linatoa fursa kubwa kwa chapa za hoteli za kimataifa kutokana na ukuaji wake endelevu wa uchumi, utulivu na kupanuka kwa kasi kwa tabaka la kati lenye mapato ya ziada.

    Ujumbe wa zaidi ya watu 300 wakiwemo watendaji wakuu kutoka hoteli mbalimbali za kimataifa, wawekezaji na wataalamu wa mambo ya fedha wanahudhuria kongamano hilo la siku tatu linalofanyika jijini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako