• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, kufuzu Afcon 2019: FKF yajadiliana na serikali kuhusu safari ya wachezaji wanaocheza nje ya nchi 9

    (GMT+08:00) 2018-10-03 10:33:25

    Shirikisho la mpira wa miguu nchini Kenya, FKF limesema kuwa bado halijawa na uhakika endapo wachezaji muhimu Victor Wanyama na Michael Olunga wataweza kushiriki katika mechi ya kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Ethiopia Oktoba 10.

    Wasi wasi huo unakuja baada ya serikali kuchelewa kutuma tiketi za safari kwa wachezaji 14 wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, na mazungumzo baina ya maafisa wa serikali na FKF yanaendelea ili walau hadi ijumaa tiketi hizo zipatikane.

    Kenya ambayo ilishinda mechi muhimu dhidi ya Ghana, sasa inatafuta ushindi muhimu mwingine katika mechi mbili dhidi ya Ethiopia moja ikichezwa Oktoba 10 nchini Ethiopia na marudio ikiwa ni baada ya siku nne nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako