• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Rais wa CAF azuru Cameroon, kujadili hatima ya AFCON 2019

    (GMT+08:00) 2018-10-03 10:35:51

    Rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad, yupo jiini Yaounde nchini Cameroon, kukutana na rais wa nchi hiyo Paul Biya.

    Ahmad, ameandama na mchezaji wa zamani wa nchi hiyo Samuel Eto'o na makamu wa pili wa rais wa CAF Constant Omari kukutana na kiongozi huyo mkongwe.

    Lengo la ziara hiyo ni kuzugumzia utayari wa Cameroon kuandaa mashindano ya bara Afrika mwaka 2019. Mashindano hayo, kwa mara ya kwanza, yatayashirikisha mataifa 24 badala ya 16.

    Ziara hii inakuja, wakati huu uongozi wa CAF ukisema haujaridhishwa na maandalizi ya Cameroon kufanikisha mashindano haya yaliyopangwa kufanyika kati ya Juni 15 hadi Julai 13 mwakani.

    Imekuwa ziara ya kwanza kwa rais Ahmad kuzuru Cameroon tangu alipomshinda Issa Hayatou, rais wa zamani wa CAF ambaye ni raia wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako