• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Matokeo ya Mechi za klabu bingwa Ulaya: Madrid yafungwa na CSKA Moscow

    (GMT+08:00) 2018-10-03 10:36:42

    Mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa ulaya, timu ya Real Madrid jana usiku imepoteza mechi baada ya kufungwa goli 1-0 ilipocheza dhidi ya CSKA Moscow nchini Urusi.

    Goli la CSKA lilifungwa na Nikola Vlasic kunako dakika ya 68 baada ya makosa yaliyofanywa na Toni Kroos aliyetaka kurudisha mpira kwa golikipa.

    Kwingineko Bayern Munich ikiwa nyumbani ilipata sare ya magoli 1-1 dhidi ya Ajax Amsterdam, AEK Athens ya Ugiriki ikifungwa magoli 3-2 nyumani na Benfica ya Ureno, Manchester City ya Uingereza ikipata ushindi wa magoli 2-1 ugenini dhidi ya Hoffenheim ya Ujerumani.

    AS Roma iliutumia vizuri uwanja wa nyumbani kwa kupata ushindi wa magoli 5-0 ilipocheza na Viktoria Plzen ya Jamhuri ya Czech nayo Juventus ikipata ushindi wa magoli matatu, yote yaliyofungwa na Paul Dybala kwenye mechi dhidi ya Young Boys Bern ya Uswisi.

    Michuano hiyo inaendelea leo, kwa mechi nane za timu kutoka makundi A, B, C na D.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako