• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uvumbuzi ni nguvu kubwa zaidi ya kuhimiza maendeleo endelevu nchini China

    (GMT+08:00) 2018-10-03 16:48:43

    Mwanzilishi ambaye pia ni mwenyekiti mtendaji wa Baraza la Uchumi wa Dunia Bw. Klaus Schwab hivi karibuni amesema, China iko njiani kujenga jamii ya uvumbuzi. Ripoti iliyotolewa na Mfuko wa Sayansi wa Marekani pia imesema, China ni nchi ya pili kwa uvumbuzi duniani, na bajeti yake katika uvumbuzi ni karibu sawa na bajeti zote za nchi za Umoja wa Ulaya.

    Katika historia ya binadamu, China ilitangulia duniani katika kiwango cha falaki, kalenda, safari za baharini, hisabati na jeshi. Uvumbuzi unaojulikana zaidi wa China ni karatasi, dira, baruti na uchapishaji. Baadaye, kutokana na uvamizi wa wakoloni na kudidimia kwa uchumi, China ilikuwa nyuma katika uvumbuzi ikilinganishwa na nchi za magharibi. Lakini tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, China imejitahidi kuendeleza uvumbuzi kwa nguvu zote. Mwaka jana, maendeleo ya sayansi yalichangia asilimia 57.5 ya maendeleo ya uchumi, huku bajeti ya utafiti wa sayansi na teknolojia ikifikia dola za kimarekani zaidi ya bilioni 257.

    Hivi sasa mapinduzi ya nne ya viwanda yanafanyika. Mapinduzi hayo haswa ni maendeleo ya akili bandia, nishati safi, teknolojia ya roboti, upashanaji habari wa Quantum, VR na teknolojia ya viumbe. Baadhi ya wataalamu wanasema, China iko katika treni ya kwanza ya mapinduzi hayo, lakini haipo kwenye sehemu ya mbele kabisa ya treni hiyo. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na jarida la "Nature" ambalo ni la ngazi ya juu zaidi la kisayansi duniani, tangu mwaka 2012, China imedumu kushika nafasi ya pili katika kiwango cha matoleo ya utafiti wa sayansi cha nchi mbalimbali duniani, na kiwango hicho cha China ni nusu ya kiwango cha Marekani. Hivyo China inapaswa kufanya juhudi kubwa zaidi.

    Kutokana na utandawazi wa uchumi duniani, hakuna nchi yoyote inayoweza kutatua masuala yote ya uvumbuzi. Rais Xi Jinping wa China aliwaambia wanasayansi mabingwa wa China kuwa, China itachagua njia maalumu ya kujitegemea katika kuendeleza uvumbuzi, huku ikijiunga na mtandao wa kimataifa wa uvumbuzi, ili kushirikiana na nchi nyingine katika shughuli za sayansi, kuchangia busara ya kichina, na kuhimiza jamii yenye mustakabali wa pamoja.

    Aidha, China imechukua uvumbuzi kama njia ya kimsingi ya kuendeleza sayansi na teknolojia. Ikiwa nchi inayowajibika, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kwa kina, ili kutoa mchango mpya kwa jaili ya maendeleo ya sayansi na mambo ya kibinadamu duniai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako