• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa bunge la Algeria asimamisha shughuli rasmi za bunge kutokana na kupingwa na wabunge

    (GMT+08:00) 2018-10-03 18:41:39

    Spika wa bunge la Algeria Bw. Said Bouhadja amesimamisha shughuli zote rasmi za bunge kutokana na shinikizo la wabunge la kumtaka ajiuzulu, lakini hajatangaza kama atajiuzulu au la ama lini shughuli hizo zitarejeshwa.

    Vyama vitano vya siasa vikiwemo muungano wa vyama viwili tawala juzi viliamua kusimamisha shughuli zote hadi Bw. Bouhadja atakapojiuzulu, pia wabunge 351 wamesaini barua ya kumpinga Bw. Bouhadja na kumtaka ajiuzulu.

    Wabunge hao wamesema bunge linaloongozwa na Bw. Bouhadja limekiuka sheria na kwa makusudi kuahirisha kupitisha miswada husika ya sheria, pia linatuhumiwa kwa uongozi mbaya na matumizi mabaya ya fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako