• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Yemen asema uchumi wa nchi hiyo uko hatarini kuvunjika

    (GMT+08:00) 2018-10-03 18:42:04

    Waziri mkuu wa Yemen Bw. Ahmed Obaid Bin Daghar amesema, kutokana na mapigano yanayoendelea na kupotea kwa fedha, uchumi wa nchi hiyo uko hatarini kuvunjika na thamani ya sarafu ya nchi hiyo Rial inaendelea kushuka.

    Bw. Daghar na maofisa wengine waandamizi wa serikali leo wamefanya mkutano maalumu wa serikali huko Riyadha, Saudi Arabia, ambapo Bw. Daghar amesema, kutokana na vurugu inayoletwa na kundi la Houthi, asilimia 85 ya fedha ya taifa zimepotea, biashara ya mafuta na gesi asili kwa nje imesimamishwa, na kuna uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.

    Bw. Daghar ameishukuru serikali ya Saudi Arabia kwa kuingiza dola milioni 200 za kimarekani katika Benki Kuu ya Yemen, huku akitaka kufanya mkutano wa uchumi haraka iwezekanavyo chini ya uongozi wa nchi za ghuba ikiwemo Saudi Arabia ili kutatua matatizo ya hivi sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako