• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Mwekezaji wa China anunua hisa katika kampuni ya ujenzi ya Home Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-03 18:51:49
    Mwekezaji wa China Zeyun Yang,mjenzi wa nyumba za Greatwall Apartments katika kaunti ya Machakos,nchini Kenya,amekuwa mbia mkuu wa kampuni iliyosajiliwa katika soko la hisa la Nairobi ya Home Afrika,baada ya kununua asilimia 8.2 za kampuni hiyo.

    Sajili zinaonyesha kuwa mwezi Agosti,Bw Yang alinunua hisa kwa jina lake na pia kupitia kampuni yake ya Erdemann Property Limited na Erdemann Company (Kenya) Limited.

    Kampuni ya Erdemann Property Ltd ilijenga nyumba za kuishi 1,140 za vyumba viwili na vitatu katika awamu tatu zinazoitwa Greatwall Apartments kwa gharama ya zaidi ya Sh3 bilioni.

    Sehemu ya mradi huo ilifadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako