• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yathibitisha ukuaji wa uchumi wa asilimia 7.2 Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-10-03 18:52:07
    Shirika la Fedha Duniani (IMF),limesisitiza kuwa uchumi wa Rwanda utakua kwa asilimia 7.2 kwa mwaka 2018,kutokana na shughuli nyingi za kiviwanda na mvua ambayo inatarajiwa kupiga jeki mavuno ya kilimo.

    Mwezi Juni mwaka huu,IMF na Benki ya Dunia zilitoa makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Rwanda hadi asilimia 7.2 kutokana na mvua ambazo taasisi hizo zinasema zimeboresha ugavi wa chakula.

    Katika robo ya kwanza ya mwaka,nchi hiyo iliandikisha ukuaji wa asilimia 10.6 katika pato la jumla la taifa.

    Rwanda ni mojawapo ya nchi zinazokuwa kwa kasi sana kiuchumi ikiwa na wastani wa asilimia 7 kila mwaka tangu mwaka 2000.

    Mkuu wa timu ya IMF,Laure Redifer,aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba baada ya kupanda hadi asilimia 6.1 mwaka jana,pato la taifa liliongezeka hadi asilimia 8.6 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018.

    Mfumuko wa bei unatarajiwa kuwa na wastani wa asilimia 2.8 kufikia mwisho wa mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako