• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria aapa kumrejesha nyumbani salama msichana aliyetekwa na Boko Haram

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:02:54

    Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari jana aliwahakikishia watu kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kumrejesha nyumbani salama msichana wa shule aliyetekwa Leah Sharibu.

    Leah Sharibu ni mkristo pekee miongoni mwa wanafunzi 110 waliotekwa wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Serikali katika mji wa Dapchi kaskazini mashariki mwa Yobe, ambaye bado anashikiliwa na Boko Haram. Kupitia mtandao wa Twitter rais Buhari alisema ameongea na mama wa msichana Bi Rebecca Sharibu na kumhakikishia kuwa serikali yake itamrejesha nyumbani salama binti yake.

    Kundi la kigaidi la Boko Haram limeripotiwa kutoa tarehe ya mwisho ambayo ni Oktoba 15 kwa serikali kukidhi mahitaji yao ili wamwachie Leah huru ama sivyo watamuua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako