• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu katibu Mkuu wa UM aonya dhidi ya vitendo vya unyanyasi wa kingono na ukatili kwa watoto duniani

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:03:19

    Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed jana alionya vitendo vya unyanyasi wa kingono na ukatili dhidi ya watoto duniani.

    Akiongea kwenye hafla ya "Kuleta Mwanga Juu ya Unyanyasi wa Kingono kwa Watoto na Ukatili" Bi Mohammed alisema kila siku katika nchi na ngazi zote za jamii, mamilioni ya wasichana na wavulana wanakabiliwa na vitendo vya unyanyasi kingono na ukatili utotoni mwao, ambavyo vinawatishia maisha yao. Amesema takriban wasichana milioni 120 duniani chini ya miaka 20 ambao ni 1 ya 10 wanalazimishwa kushiriki vitendo vya ngono.

    Wakati huohuo nchini Tanzania wimbi jipya la utekaji watoto katika mazingira ya kutatanisha limeibuka upya huku katika kipindi cha wiki mbili, watoto zaidi ya wanne wakitekwa katika jiji la Dar es Salaam hali ambayo imezidisha wasiwasi kwa wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako