• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa kanuni mpya za kuzuia kuingia kwa bidhaa zisizofikia vigezo

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:22:00

    Kenya imetoa kanuni mpya za kuzuia kuingia kwa bidhaa zisizofikia vigezo nchini humo.

    Waziri wa Ustawi wa Viwanda, Biashara na Vyama vya Ushirika Peter Munya na waziri wa Fedha na Mipango Henry Rotich wametoa taarifa ya pamoja ikisema kanuni hiyo mpya inataka bidhaa zote zitakazoingizwa Kenya zifanyiwe ukaguzi kwa lazima katika nchi zinazozalishwa au kusambazwa bidhaa hizo, na zile ambazo zimefika bandarini bila ya kufanyiwa ukaguzi hazitaruhusiwa kuingia nchini humo.

    Wamekumbusha kuwa lengo la utaratibu huo ni kuhakikisha bidhaa zinazoingia Kenya kutoka nje zinaendana na vigezo vya nchi hiyo, na kwamba bidhaa zinazopakiwa kuanzia tarehe mosi, Oktoba na baada ya hapo zinatakiwa kufuata kanuni hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako