• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rais Biya asema Cameroon iko tayari kuandaa AFCON 2019

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:36:12

    Rais wa Cameroon Paul Biya amesisitiza kuwa nchi yake iko tayari kuwa mwenyeji wa mashindano ya mataifa ya bara Afrika AFCON, yatakayofanyika mwaka 2019.

    Hakikisho hilo, limekuja baada ya rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad kukutana na rais Biya juzi Jumanne jijini Yaounde.

    Ahmad naye amesema kuwa, CAF kwasasa haina mpango wa kuondoa mashindano hayo nchini Cameroon baada ya kuhakikishiwa na rais huyo kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na yatakamilika kabla ya michuano hiyo kuanza.

    Mashindano ya mwaka ujao kwa mara ya kwanza, yatajumuisha nchi 24, kutafuta mshindi katika michuano hiyo mikubwa itakayochezwa kati ya mwezi Juni na Julai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako