• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Ethiopia aahidi kuendeleza mageuzi yaliyopo

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:38:43

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw Abiy Ahmed jana aliahidi kuendeleza mageuzi yaliyopo kwenye mkutano mkuu wa 11 wa muungano tawala wa EPRDF uliofanyika mjini Hawassa, wenye kauli mbiu ya "Mshikamano wa taifa kwa ajili ya ustawi wa pande zote".

    Shirika la habari la taifa ENA limeripoti kwamba waziri mkuu wa Ethiopia amedokeza kuwa mkutano huo mkuu utajadili matokeo yaliyopatikana katika miezi michache iliyopita kwenye sekta za uchumi wa jamii na siasa. Amesisitiza kuwa masuala ya kupunguza idadi ya watu wasio na ajira, kuimarisha uwezo wa uzalishaji, kuboresha maisha ya wananchi na kuhakikisha utawala wa kisheria yatapewa kipaumbele kwenye mkutano huo. Pia amesema Muungano tawala utaendeleza mageuzi kwa kushirikisha viongozi vijana na wale wenye uzoefu mkubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako