• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini latoa wito kupambana na mapigano ya magenge

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:46:48

    Bunge la Afrika Kusini limetoa wito wa kuweka mkakati kwa pande zote ili kupambana na vurugu za magenge zinazoongezeka kwenye baadhi ya sehemu nchini humo.

    Kamati ya polisi kwenye bunge la nchi hiyo PCP imesema kwenye taarifa kuwa, mapambano dhidi ya vurugu za magenge si kama tu ni suala la sheria bali ni mkakati wa pande wote unaohusisha idara za serikali, jamii ya umma, mashirika yasiyo ya kiserikali, biashara, taasisi za elimu, viongozi wa jamii na taasisi za kidini.

    Wito huo unakuja baada ya vurugu mpya za magenge kutokea nchini humo, haswa mjini Cape Town na mkoa wa Cape Magharibi ambapo kwa mujibu wa tawimu zilizotolewa mwezi uliopita na waziri wa Polisi Bw. Bheki Cele, mauaji ya watu 808 yaliripotiwa kati ya Aprili 1, 2017 na Aprili 31, 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako