• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Imani ya wananchi ndio ni nguvu ya taifa

    (GMT+08:00) 2018-10-04 11:06:00

    Kuanzia Oktoba mosi ambayo ni Siku ya taifa ya China, wachina wameingia kwenye kipindi cha mapumziko ya siku saba, na safari za kitalii kote nchini ni moja ya njia za kawaida kwa wachina kusherehekea siku ya taifa.

    Takwimu zinaonesha kuwa katika Oktoba mosi pekee, watalii milioni 122 wametembelea sehemu mbalimbali nchini China na kuleta mapato ya dola za kimarekani bilioni 15, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 7 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho. Takwimu hizo zinaonesha kuwa wananchi wa China wana imani na nchi yao licha ya nchi za magharibi kukadiria kushuka kwa uchumi wa China.

    Katika miaka iliyopita, China iliwahi kukabiliwa na changamoto kubwa, na kila mara ilifanikiwa kupita wakati mgumu na kuendelea kupiga hatua kubwa mbele. Viongozi wa China wanaona kuwa imani ya wananchi ndio ni nguvu na matumaini ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako