• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuangalia upya mikataba ya kimataifa dhidi yake

    (GMT+08:00) 2018-10-04 16:49:36

    Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani John Bolton amesema kuwa nchi hiyo itaangalia upya makubaliano yote ya kimataifa ambayo inaamini yanakinzana na nchi hiyo.

    Akizungumza katika ikulu ya Marekani, Bw. Bolton amesema rais wa nchi hiyo Donald Trump ameamua kuwa Marekani itajitoa kwenye Itifaki ya Hiari kuhusu Utatuzi wa Migogoro iliyofikiwa kwenye mkutano wa Vienna kuhusu Uhusiano wa Kidiplomasia. Amesema hatua hii inahusiana na kesi iliyofunguliwa na Palestina ikiitaja Marekani kama mshtakiwa, ikipinga hatua ya Marekani kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem nchini Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako