• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wateja wa China wazingatia zaidi ubora wa huduma na bidhaa

    (GMT+08:00) 2018-10-04 16:56:37

    Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi nchini China, wateja wamebadili tabia yao na kuzingatia zaidi ubora wa huduma na bidhaa.

    Utalii kwa kukodi gari unapendwa wachina wengi. Katika siku saba za mapumziko za sikukuu ya taifa, Bw. Wang kutoka mji wa Chongqing amepanga kutalii katika sehemu ya magharibi mwa mkoa wa Sichuan kwa kuendesha gari. Anasema,

    "Tuna siku saba za mapumziko, na zinatosha kwetu kufanya utalii. Pia wakati wa sikukuu ya taifa, ada ya kupita barabara kuu inasamehewa. Hivyo leo nimekuja kukodi gari."

    Takwimu zinaonesha kuwa, kabla ya Siku ya Taifa, asilimia 95 ya magari katika kampuni za kukodisha magari zimeagizwa na wateja. Wataalamu wanaona kuwa, kila mwaka, siku za mapumziko ya Siku ya Taifa ambapo hali ya hewa ni nzuri, zinakuwa ni kilele cha utalii, na zaidi ya hayo, watu wengi wanapenda kuchagua siku hizo kuwa wakati wa kufunga ndoa, hivyo soko la kukodisha magari linapamba moto.

    Siku ya Taifa pia imehimiza ustawi wa soko la utalii katika nchi za nje. Kampuni ya utalii ya Xiechen inakadiria kuwa, katika siku saba za mapumziko, idadi ya wachina wanaotalii katika nchi za nje inaweza kufikia milioni saba. Nchi na sehemu zinazopendwa zaidi na watalii wa China ni pamoja na Japan, Thailand, Korea ya Kusini, Singapore, Russia na Hongkong.

    Hivi sasa wateja wa China wamebadili tabia yao na kuzingatia zaidi ubora wa huduma na bidhaa.

    "Napenda kwenda kufanya ununulizi katika supamaketi ya hali ya juu."

    "Leo nakuja kutazama filamu. Kila wiki nakuja mara moja. Hakuna baridi wakati wa majira ya baridi na joto wakati wa majira ya joto, sipendi kucheza nje."

    Takwimu zinaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, mauzo ya tiketi za filamu yamezidi dola bilioni 4.6 za kimarekani, huku mauzo ya rejareja ya bidhaa zote yakizidi dola trilioni 2.6.

    Naibu mkurugenzi wa kituo cha uchunguzi wa ustawi wa uchumi wa idara ya takwimu ya China Bw. Pan Jiancheng amesema, matumizi yamekuwa nguvu kubwa zaidi ya kuhimiza maendeleo ya uchumi nchini China. Anasema,

    "Kwa mujibu wa hali ya soko la matumizi, mwelekeo wa kuboreshwa kwa muundo wa matumizi unaharakishwa. Kwanza, huduma zinachukua nafasi zaidi badala ya bidhaa halisi, na pili kiwango cha bidhaa na huduma zinazochaguliwa na wateja kinainuka."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako