• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waongeza idhini ya kupambana na uhamiaji haramu na magendo ya binadamu nchini Libya

    (GMT+08:00) 2018-10-04 17:13:41

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio namba 2437 na kuamua kuongeza miezi 12 ya muda wa kupambana na uhamiaji haramu na magendo ya binadamu kupitia eneo la bahari ya Mediteranin nchini Libya.

    Amizio hilo limepitishwa kwa kura zote 15 za ndiyo na kuongeza muda huo hadi Oktoba 3 mwaka 2019.

    Habari nyingine zinasema, Libya imeshirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji kuwarejesha nyumbani wahamiaji haramu 96 kutoka Bangladesh na Pakistan.

    Idara ya kupambana na magendo ya binadamu ya Libya imesema, wahamiaji hao wamerejeshwa makwao kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli, ambao 60 kati yao walitoka Bangladesh na wengine 36 walitoka Pakistan. Urejeshaji huo ni sehemu ya operesheni ya kurejeshwa kwa hiari inayotekelezwa na serikali ya Libya na shirika la kimataifa la uhamiaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako