• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Zabuni ya Kenya Power yazua utata

    (GMT+08:00) 2018-10-04 18:11:15

    Sakata la uteuzi wa kampuni ya kutoa huduma za uchukuzi na uwekezaji kwa Kenya Power (KP) imeudhi Benki ya Dunia (WB), mashirika ya kutoa misaada ya kimataifa, Bunge la Seneti na Kitaifa, mahakama inayosikiza kesi za ufisadi ilifahamishwa ..

    Meneja mkuu wa ukaguzi wa KP Bw Charles Cheruiyot Kipng'eno alisema kampuni nyingi ambazo hazikuwa zimewasilisha maombi ya kutoa huduma za uchukuzi na uwekezaji (L&T) ziliteuliwa.

    Bw Kipng'eno alisema kuwa kampuni hizo ziliorodheshwa baada ya ufunguzi wa zabuni na wanachama wawili wa kamati hiyo Bw Bernard Githui Muturi na Mhandisi Evelyne Pauline Amondi.

    Meneja huyo alisema zabuni hiyo haikupasa kufunguliwa na wanachama wawili kama ilivyofanywa na Bw Muturi na Bi Amondi.

    Mwanachama wa tatu wa kamati hiyo Bw David Makenzi aliyekuwa ameteuliwa na Mkurugenzi mkuu wa KP Dkt Ken Tarus hakufika wakati.

    Walioshtakiwa ni Dkt Tarus, wahandisi Harun Karisa, Daniel Tare, Noah Ogano O Omondi, Daniel Ochieng Muga, John Mwaura Njehia, James Muriuki, Bw Muturi na Bi Amondi.

    Wote tisa wanakabiliwa na shtaka la kuidhinisha makampuni ambayo hayakuwa yamehitimu kutoa huduma za L&T na kupelekea KP kupoteza zaidi ya Sh159 milioni.

    Wamekana waliidhinisha kampuni hizo kati ya Aprili 12, 2017 na Juni 12, 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako