• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wauzaji Unga wa sima wakaidi bei ya 75

    (GMT+08:00) 2018-10-04 18:11:34

    Licha ya waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri kuonya wafanyabiashara wanaouza unga wa mahindi kwa bei ya juu kuwa kuwa watakamatwa na kushtakiwa,utafiti wetu umedhihirisha kwamba idadi kubwa ya wafanyibiashara hao hawajabadilisha bei mpaka sasa.

    Waziri alisema wafanyabiashara ni sharti wauze kilo mbili za unga wa mahindi kwa Sh75 huku akisisitiza kuwa hilo halitakuwa na mjadala.

    Wafanayibiashara ho wa reja reja wamedai eti wataanza kutumia bei hiyo mpya pale watakapokamilisha unga waliouziwa kwa bei ya juu.

    Wanasema itakuwa ni hasara kwao kuuza kwa bei mpya ilhali wamenunua unga huo kwa bei ya jumla ya awali kabla ya agizo.

    Waziri wa kilimo alisisitiza kwamba hawataruhusu Wakenya kupunjwa na viwanda vya kusaga unga wa mahindi pamoja na wafanyabiashara walaghai.

    Hata hivyo, agizo hilo la Bw Kiunjuri huenda likagonga mwamba kwani Kenya ni soko huru ambapo wafanyabiashara wanajiamulia bei ya bidhaa zao.

    Lakini waziri alishikilia kuwa kwa sasa mahindi yanauzwa kwa bei ya chini hivyo unga pia unastahili kuuzwa kwa bei nafuu.

    Alisema hatua ya serikali kuweka bei ya unga inalenga kuhakikisha kuwa watumiaji wa unga wanalindwa dhidi ya wafanyabiashara walaghai wanaouza bidhaa hiyo kwa bei ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako