• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Benki ya dunia yakosoa marekebisho ya sheria ya takwimu

    (GMT+08:00) 2018-10-04 18:12:15

    Benki ya dunia hiyo haikuridhishwa marekebisho ya sheria yanayopendekezwa kufanywa kwenye Sheria ya Takwimu ya 2015 nchini Tanzania.

    Kupitia kwa taarifa yake ,benki hiyo inasema sheria hizo haziendani na viwango vya kimataifa vilivyowekwa kuhusu takwimu.

    Imeelezea kwamba wameifahamisha Tanzania kwamba marekebisho hayo, iwapo yatatekelezwa, huenda yakaathiri sana kuandaliwa kwa takwimu rasmi na zisizo rasmi, ambazo huwa muhimu sana kwa ustawi wa taifa lolote lile.

    Benki hiyo inajadiliana na serikali ya Tanzania kuhusu utoaji wa msaada zaidi katika kujenga mifumo ya takwimu endelevu unafaa kwa wakati huu.

    Aidha mashauriano yanaendelea na kwamba wameeleza wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo ya takwimu, lakini haijasitisha mradi huo.

    Kadhalika, kiasi hicho cha $50 milioni bado kimeorodheshwa kwenye tovuti ya benki hiyo kama msaada unaopangiwa kutolewa kwa Tanzania, ingawa mpango huo bado haujaidhinishwa, bado upo kwenye utaratibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako