• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Mfumko wa uchumi waongezeka Uganda

    (GMT+08:00) 2018-10-04 18:12:31
    Mfumko wa uchumi na bei ya bidhaa na gharama ya maisha kwa jumla nchini Uganda vimeendelea kushuhudiwa mwezi wa Septemba na Oktoba.

    Benki kuu ya Uganda imesema kiwango cha riba kwa benki za biashara kwa kiasi cha asilimia 10, ikiwa ongezeko la juu zaidi kwa mda wa miaka mitatu,itazua hofu kwamba huenda nchi hiyo ikakumbwa na mfuko wa juu wa gharama ya maisha.

    Gavana wa benki kuu ya Uganda Prof Emmanuel Tmusiime Mutebile, amesema kwamba mfumko wa fedha unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5 zaidi katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

    Amesema kwamba hatua ya benki kuu kuongeza kiwango cha riba ilitarajiwa, wakati bei ya mafuta ikitarajiwa kuongezeka zaidi kati ka historia ya nchi hiyo na kufikia shilingi 5000 kwa kila lita ya mafuta ya petrol kutoka shilingi 3500 za sasa.

    Wananchi wa Uganda aidha wamekabiliwa na hali ngumu ya miasha huku wengi wao wakiishi chini ya dola moja kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako