• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ronaldo aachwa timu ya taifa kutokana na tuhuma zinazomkabili

  (GMT+08:00) 2018-10-05 08:28:53

  Mshambuliaji Cristiano Ronaldo wa Ureno ametemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kitakachomenyana na Poland na Scotland baadaye mwezi huu.

  Nyota huyo wa Juventus, ambaye ameifungia timu yake ya taifa mabao 85 katika mechi 154, hajaitwa kwenye kikosi cha michuano ya ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Poland na wa kirafiki dhidi ya Scotland.

  Kocha wa Ureno Fernando Santos ameweka bayana kutomuita Ronaldo katika kikosi hicho kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuwasiliana na Ronaldo na Mkuu wa Chama cha Soka Ureno.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako