• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina imani kubwa katika kuzinufaisha nchi nyingi duniani kutokana na maendeleo yake

    (GMT+08:00) 2018-10-05 10:01:20

    Katika kikao cha 73 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kilichomalizika hivi karibuni, rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena alishikilia wito wake wa "Marekani Kwanza" na kudai kupinga mfumo wa usimamizi wa dunia nzima, kauli ambayo imelaumiwa na viongozi wa nchi nyingi wakiwemo wenzi wake wa jadi.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Matiafa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa viongozi na wajumbe waandamizi kutoka nchi mbalimbali waenzi moyo wa ushirikiano, na kutafuta ufumbuzi wa masuala muhimu duniani.

    Hivi karibuni, hatua za kujitenga na pande nyingine, na za upande mmoja zimezidi kuongezeka katika baadhi ya nchi zilizoendelea, hali ambayo imeleta shinikizo kubwa kwa ushirikiano wa kimataifa na usimamizi wa dunia nzima. Namna ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja katika dunia inayokabiliwa na mfarakano, ni masuala muhimu yanayojadiliwa zaidi katika mikutano muhimu duniani likiwemo baraza la uchumi la dunia la Davos na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, wakati huo huo mapendekezo yenye busara yaliyotolewa na China yamefurahiwa na kupongezwa na jumuiya ya kimataifa.

    Mwanataaluma maarufu wa Marekani Robert Kuhn alipohojiwa miaka miwili iliyopita alisifu pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" lililotolewa na rais Xi Jinping wa China mwaka 2013, akisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa China kujihusisha katika mambo ya kimataifa, na ni mchango muhimu katika kuhimiza maendeleo ya dunia nzima.

    Katika kikao cha 73 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje na uchumi wa nje wa Hungary Bw. Peter Szijjarto pia amesifu sana pendekezo hilo la China, akisema kuwa mitaji kutoka Mashariki haswa kutoka China imeziletea nchi za magharibi teknolojia za kiwango cha juu. Pia amefurahia kwa Hungary kuchukua fursa hiyo na kujenga miundo mbinu inayoiunganisha Hungary na nchi nyingine kwa kuvutia uwekezaji kutoka China. Kwa maoni yake utaratibu mpya wa dunia uko mbioni kuundwa.

    Ili kukabiliana na mafungamano ya kiuchumi duniani, China iliyotekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa zaidi ya miaka 40, itaendelea kushikilia sera hiyo iwe msukumo wake wa kupata maendeleo, na hakika italeta fursa nyingi zaidi kwa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako