• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga shutuma zisizo na msingi kutoka Marekani

    (GMT+08:00) 2018-10-05 10:16:09

    China imeeleza kupinga shutuma zisizo na msingi dhidi ya sera zake za ndani na nje baada ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence jana kuishutumu China kuingilia mambo ya ndani na uchaguzi wa Marekani, na kuzikosoa sera za ndani na nje za China.

    Hayo yamesemwa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying ambaye pia amesema wananchi wa China wana imani kubwa na ujamaa wenye umaalum wa kichina, na historia na hali halisi vimeonyesha kuwa hii ni njia ya mafanikio inayolingana na hali ya China, na inayoweza kutimiza ustawi wa taifa na neema ya wananchi. Ameongeza kuwa China imepata maendeleo makubwa kutokana na juhudi za wananchi wake, pia kutokana na ushirikiano wa kusaidiana na kunufaishana na nchi mbalimbali duniani, lakini sio kwa utoaji sadaka wa watu wengine.

    Amesisitiza kuwa China siku zote inashikilia kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na haina nia ya kuingilia sera ya ndani na uchaguzi wa Marekani, pia jumuiya ya kimataifa inatambua vya kutosha ni nchi ipi inayopenda kukiuka mamlaka, kuingilia kati na kuharibu maslahi ya nchi nyingine. Amesema China inaitaka Marekani iache kuishutumu China bila ya msingi, na kuchukua hatua za kivitendo kulinda uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako