• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza mkakati mpya wa kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2018-10-05 17:07:02

    Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani John Bolton amesema nchi hiyo imeandaa mkakati mpya wa kupambana na ugaidi ambao unazingatia zaidi ulinzi wa ndani, kuzuia mashambulizi na kupunguza hasara baada ya kushambuliwa.

    Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani imesema, mkakati huo una malengo muhimu ya kupunguza uwezo wa magaidi kushambulia Marekani na vituo vya nchi hiyo duniani, kukata chanzo cha ufadhili kwa makundi ya kigaidi, na kupunguza uwezo wa magaidi kuenea siasa za msimamo mkali nchini humo. Pia itahakikisha magaidi hawapati silaha za maangamizi, kulinda na kuwaepusha wamarekani kukumbwa na shambulizi la ugaidi na kuhimiza idara ya umma na ya binafsi na wenzi wa kimataifa katika kupambana na ugaidi.

    Mkakati huo umeitaja Iran kama nchi inayounga mkono zaidi ugaidi, nakuonesha kwamba, serikali ya Marekani inajaribu kuzuia Iran kuongeza ushawishi katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako