• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China chafungua taasisi na madarasa ya Confucius katika nchi na sehemu 149 duniani

    (GMT+08:00) 2018-10-05 17:19:20

    China imefungua taasisi 530 na madarasa 1,113 ya Confucius katika nchi na sehemu 149 kote duniani.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya taasisi ya Confucius katika Siku ya Kutembeleamakao hayo, hivi sasa walimu 46,200 walioajiriwa na wa mikataba wanafanya kazi katika taasisi na madarasa ya Confucius, na wanafunzi zaidi ya milioni 9 wamefundishwa katika taasisi na madarasa hayo.

    Katika siku hiyo, makao makuu ya taasisi ya Confucius yamewasiliana nataasisi zake 7 barani Asia, Oceania, Afrika na Ulaya kupitia video, na kuonesha maeneo mbalimbali ya mafunzo na shughuli maalumu za kiutamaduni.

    Shughuli hiyo imehudhuriwa na watu 400 wakiwemo mabalozi kutoka nchi mbalimbali nchini China, wajumbe kutoka mashirika ya utamaduni ya nchi za nje, na shule za China zinazoshirikiana na taasisi ya Confucius.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako