• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatoa onyo kali kwa watumishi wa TRA

    (GMT+08:00) 2018-10-05 18:59:38

    Waziri wa Fedha na Mipango Bw. Philip Mpango ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu wafanyakazi wake wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo rushwa na kutumia njia zisizokubalika wakati wa kukusanya kodi za Serikali.

    Akizungumza na wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Tanga, Mpango ameagiza TRA kuhakikisha wafanyakazi wake wanafanya kazi ipasavyo na kuwaondoa wanaokiuka kanuni na maadili ya kazi. Kauli hiyo inakuja kufuatia madai kuwa baadhi ya wafanya kazi wa TRA wamehusishwa na tuhuma za ulevi wa kupindukia na kujihusisha na mtandao wa wafanyabiashara unaotumika kuikosesha Serikali mapato yake

    Amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kuwa waadilifu kwa kujiepusha na vitendo vya rushwa na lugha za kuudhi kwa wateja wao ili kupunguza malalamiko kutoka kwa walipa kodi na kuonya kuwa serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayefanya kazi kinyume na maadili ili kujenga nidhamu kwa watumishi hao na hatimaye kuongeza ufanisi katika ukusanyaji mapato ya Serikali. Aidha TRA imeongeza kuwa inashirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoa elimu kuhusu maadili mema ya kazi na kuwachukulia hatua kali watumishi wanaobainika kujihusisha na vitendo vinavyochafua taswira ya TRA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako