• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nusu ya mapato hutumika kulipa madeni

  (GMT+08:00) 2018-10-05 19:00:03

  Serikali ya Kenya inadaiwa kutumia zaidi ya nusu ya mapato yote nchini humo kulipia madeni.

  Kwa mujibu wa ripoti ya Hazina kuu nchini Kenya, Kati ya Sh100 zinazopatikana na Hazina Kuu kati ya Julai na Agosti, Sh57 hutumiwa kulipa madeni.

  Kutokana na kulipwa kwa madeni, serikali ilitumia Sh118.08 katika muda wa miezi miwili ya mwanzo katika mwaka huu wa kifedha kulipa madeni.

  Katika kipindi kama hicho mwaka jana, serikali ilitumia Sh35.08 bilioni kulipa madeni. Waziri wa Fedha Henry Rotich alisema hayo katika ripoti ya hivi punde kuhusu mapato ya serikali.

  Kiwango cha madeni kimekuwa cha juu kikilinganishwa na kiwango cha mapato ya serikali, hasa kutokana na kuwa mikopo iliyochukuliwa miaka mitano iliyopita imekomaa na imeanza kulipwa.

  Kutokana na hilo, utoaji wa fedha kwa miradi umekuwa balaa ikizingatiwa kuwa kaunti 32 kati ya 47 hazikupokea mgawo wazo kutoka kwa serikali ya kitaifa katika kipindi hicho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako