• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga lawama ya kiongozi wa Marekani isiyo na msingi wowote

    (GMT+08:00) 2018-10-05 19:00:29

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Hua Chunying amepinga kauli iliyotolewa na Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence dhidi ya China juu ya masuala ya Taiwan, bahari ya kusini, haki za binadamu na dini.

    Bibi Hua Chunying amesema, kuna China moja tu duniani, na Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China, na Marekani haina mamlaka ya kutoa hoja yoyote kuhusu nchi husika kuendeleza uhusiano na China chini ya msingi wa sera ya China Moja.

    Bibi Hua pia amesisitiza tena kuwa, China ina mamlaka halali katika visiwa vya Bahari ya Kusini na maeneo ya bahari yaliyoko karibuna ujenzi wa vituo vya ulinzi wa taifa vinavyohitajika katika ardhi yake unafuata haki ya kujilinda inayopewa na sheria za kimataifa, ambako hakuna uhusiano na kuongeza nguvu ya kijeshi.

    Wakati huohuo, Bibi Hua pia amesema kuwa serikali ya China inatilia maanani katika kulinda na kuhimiza haki za binadamu, na kwamba watu kutoka kabila mbalimbali wana uhuru wa dini kwa kufuata sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako